MBUNGE TIM WANYONYI ASISITIZA UCHAGUZI WA 2017 USIAHIRISHWE

Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi 

Mbunge wa Westlands jijini Nairobi Timothy Wanyonyi amepinga hoja ya kuahirisha tarehe ya uchaguzi mkuu ujao inayopania kuwapa wabunge muda zaidi wa kuhudumu bungeni.
Mbunge huyo alisema hayo Alhamisi katika Taasisi ya Mafunzo ya KTTC alipokuwa akihudhuria hafla ya kuadhimisha mwaka wa pili tangu vikundi vya akina mama vya kuchangisha fedha katika eneo hilo kuanzishwa.
"Sisi kama mrengo wa Cord hatuungi mkono pendekezo la kuongeza muda wa kuhudumu kwa bunge au wabunge. Tunataka uchaguzi ufanyike Agosti mwakani. Isiwe kabla wala baada ya hapo, kama ilivyonakiliwa kisheria. Nasi tuko tayari kwa ajili ya uchaguzi,” alisema Bw Wanyonyi.



Kutilia mkazo

Akiandamana naye gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero alitilia mkazo suala hilo na kuwashauri viongozi waache ubinafsi.
“Jamani viongozi tusitafute viti kwa ajili ya maslahi yetu wenyewe bali tuzingatie matakwa ya umma,” alisema Dkt Kidero.
Bw Wanyonyi aliyedhihirisha azma yake ya kuwania ugavana wa Nairobi mwaka 2022 pia aliishambulia serikali na kuwaonya dhidi ya kuingilia michakato ya mrengo wao wa Cord.
“Hakuna sheria inayosema IEBC sharti isimamie chaguzi kwenye vyama mbalimbali. Nasi kama Cord tukitaka watusaidie kuandaa chaguzi zetu tutaamua kwa hiari yetu lakini serikali haiwezi kutulazimisha kufanya hivyo. Wala hatuungi mkono hatua hiyo iliyochukuliwa na wapinzani wetu,” alisisitiza Bw Wanyonyi.
Mbunge huyo wa Westlands pia aliwahimiza makamishna wapya watakaoteuliwa kuisimamia IEBC ‘wasafishe’ sajili iliyopo ya wapiga kura na kuwasajili wapiga kura wapya kwa shime kabla ya Cord kupambana na mahasimu wao debeni bila ya ubaguzi.
“Wapinzani wetu hawatubabaishi. Eti wamesema watatupanga, watatupanga vipi na sisi ndio serikali hapa Nairobi? Sisi ndio tutawapanga!” Bw Wanyonyi alifoka.

Comments

  1. By numbers we prevail, by popularity our figures speak for themselves, by voices our reasons are absolute. Cord is not just an individual but an institution. Hon Tim wanyonyi my MP tell them

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MP TIM WANYONYI LEADS IN HARAMBEE FOR CONSTRUCTION OF NEW DORMITORY AT PARKLANDS ARYA GIRLS

KANGEMI PRIMARY TRANSFORMED BY TIM WANYONYI

THOUSANDS OF KIBAGARE SLUM DWELLERS IN WESTLANDS FACE POTENTIAL EVICTIONS